This site offers materials from Bende, Katavi Region, Tanzania
 IRC & LingDy 2
ILCAA, Tokyo University of Foreign Studies

Home Introduction Tusahule Sibhende
Dictionary

Unit 17  Suula jye ekumi na ndwi

Mighanyi jya Sibhende / Methali za Kibende

* Methali nyingi katika sura hii zimetolewa kutoka “Mighaɲi Ja Sibhēnde - Methali za Kibende” © SIL-International 2012.

   Alino kubhoko kuleehe. 
Tafsiri:  Ana mkono mrefu. 
Maelezo:  Yeye ni mwizi. 
Bhulanda bhwa nsoka bhulyasya na ndaa. 
Tafsiri:  Huzuni ya nyoka ni kutembelea na tumbo. 
Maelezo:  Ana tamaa ya kupata vizuri ila uwezo (pesa) hana.
Fikulu fikuleenwe / fisumbeene. 
Tafsiri:  Vikubwa vinazidiana. 
Maelezo:  Hakuna mkuu asiye na mkuu wake. 
Ghooghu muntu tyakoolaala na mwambi mundaa. 
Tafsiri:  Mtu halali na mshale tumboni. 
Maelezo:  Binadamu hana siri. 
Ghwasanga iitili lili kusiti sanga lyatansibhwanga. 
Tafsiri:  Ukimkuta kobe yuko kwenye mti ujue amepandishwa. 
Maelezo:  Ukiona mtu amepewa cheo ambacho hana uwezo nacho ujue kapendelewa. 
Ghwatuka mukulu sanga ghwaliniela. 
Tafsiri:  Ukimtukana mkubwa ujue umejinyea. 
Maelezo:  Usimtukane mtu mkubwa utapata matatizo. / Usitukane mamba kabla hujavuka mto. 
Iikala lisinateemwi likooja lifyonwele. 
Tafsiri:  Nguchiro ambaye hajawahi kukatwa, huenda uchi. 
Maelezo:  Mtu ambaye hajawahi kupata matatizo hawi makini. 
Jya bhukwe jikoolibhwa bhwinama. 
Tafsiri:  Ukikirimiwa ukweni hula kwa aibu. 
Maelezo:  Ukitaka kufanikiwa lazima uwe mvumilivu. 
Jyabhuulila tejikoolyana. 
Tafsiri:  Kilichodhihirika hakiangamizi. 
Maelezo:  Tatizo lililojulikana ni rahisi kulitatua. Mchawi mpe mwana alee. 
Jyabhonda mulomo tejikoolesya jindi kupala. 
Tafsiri:  Iliyopondeka mdomo haikatazi mwingine kutafuta. 
Maelezo:  Tatizo la mtu mwingine halikuzuii wewe kutafuta. Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji. 
Kaaminula musila mwitimba munkungwe kaatumpe eghulu. 
Tafsiri:  Mnyama mdogo (wa ngiri) anaweza kubinua mkia porini akagusa anga. 
Maelezo:  Mtu akionyesha tabia mbaya mwanzoni, mwishoni itakuwa zaidi. 
Kaatamba mbulu musila na managha keebhwene. 
Tafsiri:  Kinachovuta kenge mkia kinajiona kina nguvu. 
Maelezo:  Mtu hawezi kufanya jambo lililo nje ya uwezo wake. 
Kaatete efuha habhugheni hamwabho kamile esima. 
Tafsiri:  (Kitu kidogo) kinachouma mfupa ugenini kwao kinameza zima. 
Maelezo:  Mtu anayeshindwa kuzuia tabia yake ugenini basi nyumbani kwake atakuwa na tabia mbaya zaidi. Ukienda ugenini kuwa makini. 
Kaa ghundi kaalyohela kunkookola. 
Tafsiri:  Cha mwingine hupendeza mwilini. 
Maelezo:  Mali ya mtu mwingine haina faida kwako. Cha kuazima hakisitiri matako. 
Kaliilabhila kakoonywa mabhenge. 
Tafsiri:  Kilichoamka mapema hunywa maji safi. 
Maelezo:  Yule aliyewahi hupata kitu kizuri ndiye mjanja. 
Kalomo na kalomo kajiile kunjihasya. 
Tafsiri:  Mdomo na mdomo unapelekea kuniua. 
Maelezo:  Uongo ukizidi mwisho unaua. Mdomo huponza kichwa. 
Kalonda kaamanya nyene. 
Tafsiri:  Kidonda hukijua mwenyewe. 
Maelezo:  Shida huijua mwenye shida. Hadhabu ya kaburi aijuae maiti. 
Kanyonyi kasinalole esaka kakoofwila kwihumbu iituhu. 
Tafsiri:  Ndege ambaye hajawahi kuona mtama hufia kwenye mapepe matupu. 
Maelezo:  Kijana ambaye hajawahi kuona msichana mzuri wa rika lake huishia kuoa mzee. Tafuta msichana mdogo ili upate uzao.
Katende kakookula habhwisa bhwaje. 
Tafsiri:  Ndege (mdogo) hukua kwenye kiota chake. 
Maelezo:  Kila kitu ni bora mahali pake. 
Katende hokanywamile ghobhwano. 
Tafsiri:  Ndege (mdogo) alipopewa uzito huanikiwa kwenye chano. 
Maelezo:  Kila kitu ni bora mahali pake. 
Katwana katuniile kulufuno kakootwala siti bhuhinga. 
Tafsiri:  Kijana anayekataa (kufanya kazi) kwenye sehemu ya ujenzi mpya huchukua mti upande. 
Maelezo:  Asiyependa kufanya kazi hawi makini kwenye kazi yake. 
Kulya kwa mbwa kuli mumaghulu. 
Tafsiri:  Kula kwa mbwa (kula kokote) kunategemea miguu. 
Maelezo:  Riziki ya mbwa iko miguuni mwake. Mtembezi hula miguu yake. Mtu anayetembea hakosi riziki. Mkaa bure si sawa na mtembea bure. 
Kutusya mwegho gho kulya kahiile. 
Tafsiri:  Kutuliza moyo ndio kula kalikoiva. 
Maelezo:  Mvumilivu hula mbivu. Subira yavuta heri. Ukizidi kusubiri utapata kitu kamili. 
Kutwi kwa mbusi kukoohulika kuli munkono. 
Tafsiri:  Sikio la mbuzi linasikia likiwa chunguni. 
Maelezo:  Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Asiyesikia ushauri wa watu mwishowe atapata matatizo. 
Kwa musala tekubhuli kasunule ekosi. 
Tafsiri:  Kwa mtafutaji hakukosi kurefusha shingo. 
Maelezo:  Hata tajiri anaweza kuomba msaada kwa maskini. 
Liinso ni lisila lufumba. 
Tafsiri:  Jicho halina mpaka. 
Maelezo:  Jicho linaona mambo yote. Macho hayana panzia. 
Lwendo lwa musya lukoolyohela munsila. 
Tafsiri:  Safari ya mtumwa huwa nzuri njiani. 
Maelezo:  Mwanzo mgumu. 
Matwi teghakoolaala na nsala. 
Tafsiri:  Masikio hayalali na njaa. 
Maelezo:  Masikio husikia chochote kisemwacho. 
Mughoosi mukulu ni syala. 
Tafsiri:  Mtu mkubwa ni jalala. 
Maelezo:  Mtu mkubwa hupokea matatizo ya kila namna kutoka kwa watu. Ukubwa jalala. 
Mughongo nyuma teghukoosighwa mafuta. 
Tafsiri:  Mgongo nyuma haupakwi mafuta. 
Maelezo:  Huwezi kuyajua yanayotendeka nyuma yako. Mla mla leo mla jana kala nini. 
Mumunika nsoka akoosumbulila mumaghulu bhanda. 
Tafsiri:  Anayemmulika nyoka huanzia miguuni mwake. 
Maelezo:  Huwezi kutangaza amani bila kuanzia kwako. 
Nfula tejikooghwa lumwi. 
Tafsiri:  Mvua hainyeshi mara moja. 
Maelezo:  Shida haiji mara moja. Haba na haba hujaza kibaba. 
Sikulu tesibhuli nyene Tanganyiika ni jya Bhasobha. 
Tafsiri:  Kikubwa hakikosi mwenyewe Tanganyika ni ya (watu) wa Soba. 
Maelezo:  Hakuna himaya isiyokuwa na mwenyewe. 
Tyakoolola kaahona kwifi mpaka akakanokole. 
Tafsiri:  Haoni (kitu kidogo) hata kikianguka kwenye mavi mpaka akidonoe. 
Maelezo:  Anaokota kila akionacho. Mtu mwenye tamaa. 



Syule jya sekondaali jye eLandamilumba (Shule ya sekondari ya Lamdamilumba)

Copyright 2016 (c) Yuko ABE, All rights reserved.