This site offers materials from Bende, Katavi Region, Tanzania
 IRC & LingDy 2
ILCAA, Tokyo University of Foreign Studies

Home Introduction Tusahule Sibhende
Dictionary

Unit 15  Suula jye ekumi ne etaanu

Kamughyenyi

Kamughenyi kaa Libhugha ne Nsofu / Hadithi ya Mrarusanda na Tembo

Ukale hakabeele Libhugha ne Nsofu. Libhugha likabheele liteesile maji muntaakala.
Lindi ifuku syajise Nsofu syahuulwa ne nfula, sibhwene habhoobholi lyonsi lilikufunka. Kundi Nsofu nkulu jyatuma Nsofu nsensense kubhala,
-- Mutwana, kaje haahali, ukaleete mulilo twighanikisye.
Kalya Kasofu kaabhuuka, kuja halya hakali Libhugha. Kundi Libhugha lyalola Nsofu jilikwisa. Kundi Libhugha lyasumbula kulombe Nsofu,
-- Gwafwo oghwe, ghwafwo oghwe !
Kundi Nsofu jyaghubhaha jyaheleela mpaka kwa ghulya mughoosi mukulu ghaamutumanga. Ghaajibhasya,
-- Bhuti ?
Kundi jyatenda ti,
-- Libhugha lyanombanga ti, ‘Ghwafwo oghwe !’
Kundi naaheleela.
-- Aao ?
-- Ee.
Kundi jyatuma ghundi,
-- Kajo oghwe !
Maana mwinoobhe ghaaghubhaha. Kundi ghoogholi mukulu ghaaja, kufikaho lyamulomba bhoobhooe. Jilya Nsofu kabhili jyaheleela. Jilikuheleela jyalomba ti,
-- Ghaanomba ‘Ghwafwo oghwe !’ No one nangubhaha kufwa, bhonanheleela.
Jyabhala,
-- Kenjo ne mughoosi mukulu.
Kundi jyabhuuka kufika haali lyeleli Libhugha bhwenge bhwaje. Kundi lyasumbula,
-- Ghwafwo oghwe, ghwafwo oghwe !
Jilya Nsofu nkulu tejyakaghubhaha ghaagho maghambo. Tu bhojyajangae mpaka halya holili Libhugha. Kundi jyalitaghalala Libhugha, lyabha mumantaghalalwa. Kundi Libhugha lyatuumuka kukilima. Kundi lyatenda ti,
-- Nsofu jyantaghalala.
Kundi Nsofu jyatwala mulilo. Ghoajibheele jihensile. Jyaheleela kukali bheenaaje mukeeghanikisya.
Hapo zamani palikuwa Mrarusanda na Tembo. Mrarusanda alikuwa ametaga mayai mwenye majani makavu.
Siku moja wakaja tembo wamenyeshewa na mvua, wakaona kwa mbali moshi unafuka. Tembo mkubwa akamtuma tembo mdogo akasema,
-- Mtoto, nenda pale ukalete moto tuote.
Kale katembo kakaondoka kwenda pale alipo Mrarusanda. Mrarusanda alipoona tembo anakuja akaanza kumwambia,
-- Umekufa wewe, umekufa wewe !
Yule tembo mtoto akaogopa akarudi kwa yule tembo mkubwa aliyemtuma. Akamuuliza,
-- Vipi ?
Tembo mtoto akasema,
-- Mrarusanda ameniambia ‘Umekufa wewe !’ ndio nikarudi.
-- Kweli ?
-- Kweli.
Kwa kuwa mwenzie aliogopa hivyo akaenda mwingine. Kufika pale Mrarusanda akamwambia hivyohivyo. Yule tembo pia akarudi. Aliporudi akasema,
-- Ngoja niende mimi, mwanaume mkubwa.
Basi akaondoka. Kufika pale yule Mrarusanda kama kawaida yake akaanza,
-- Umekufa wewe, umekufa wewe !
Yule tembo mkubwa hakuyaogopa yale maneno. Akazidi kwenda tu, mpaka pale alipo Mrarusanda. Tembo akamkalia Mrarusanda, akawa chini ya miguu yake. Mrarusanda akachomoka kukimbia akisema,
-- Tembo ameniweka chini ya miguu yake.
Kisha tembo akachukua moto aliokuwa anautafuta. Akarudi kwa wenzake ili waote.



Liibhugha ne Nsofu / Mrarusanda na Tembo

Copyright 2016 (c) Yuko ABE, All rights reserved.