Unit 8 |
Suula jya munaane |
|
Monga ghwa Katuma /Mto wa Katuma |
|
Monga ghwa Katuma ni monga mukulu nkana. Bhantu bhengi nkana bhekeele
bhakungiile ghoogho mongae. Bhantu bhengi bhakooghukolela milimo mingi
nkana.
Bhakeema bhakoohalamuka mulaabho, bhaaja mukataha mansi ghaa kunywa.
Mumasyubha kubha ghwajako kumonga uloosangako bhantu bhengi nkana. Kilo
ogho na mulimo ghwa kumwaje. Bhatwana bhalikunyaagha, bhandi
bhalikukansa, bhandi bhalikugholelela bhusitaani. Yaani kilo ogho no
mulimo ghwaje.
Kubha syafike nsa sya mugholo, bhaataha mansi uloobhasanga, bheekutaha
mansi ghaa kunyaagha. Bhandi bhalikulobha masembe ne nsonfi.
Bhatunga-ng’ombe na agho bhateghemeele ghoogho mongae kunywesya fitungwa
fyabho. Kumwi na bhaahita-nsila bhakoohita bhaanywa mansi moomoe.
Ghooghu monga ni mukulu teghukookama, aajeehi. Kusogho ne sihwa ghwene
tu kujelae. Kubha kwafika kusogho, mansi ghakoofula. Yaani monga
ghukoobhumbika nkana. Kubha jyaghwe nfula kutunde, kundi monga
ghwabhumbika. Kubha syafike esihwa, ghukoohooka mansi ghaaseeha. Kubha
mansi ghaaseeha, kundi bhantu bhaaja kulima fya kulima moomo mwikata lya
ghoogho monga. Bhaalima kabhenga, mabhotebhote, fisaka fya sihwa ne
findi fingi. Kila muntu ne mbuto jyoghaateha kulima.
Kwa hiyo milimo jya ghooghu monga ni mingi. Tyonakobhola kujitenda
jyonse. Ghwajihwa, aajeehi. Tu kubha jyoghwakobhola kutenda jyoghwatenda
kobhe jyeji jyonaantenda.
|
|
Mto wa Katuma ni mto mkubwa sana. Watu wengi sana wamekaa wanaangalia mto huu. Wanafanyia kazi nyingi sana kutokana na mto huu.
Wanawake wakiamka asubuhi wanakwenda kuteka maji ya kunywa.
Mchana kama ukienda huko mtoni utakuta watu wengi sana. Kila mtu na kazi
yake. Watoto wanaoga, wengine wanafua, wengine wanamwagilia bustani.
Yaani kila mtu ana kazi yake.
Kama zikifika saa za jioni, wateka maji utawakuta wanateka maji ya kuoga. Wengine wanavua samaki na kambare.
Wafuga ng’ombe nao wanategemea mto huo kunywesha mifugo yao. Wapita njia pia hunywa maji hapo.
Mto huu ni mkubwa huwa haukauki. Masika na kiangazi
yenyewe unatembea tu. Kama ikifika masika maji huwa mengi. Yaani mto
unajaa sana. Kama ikipiga mvua huko juu mto unajaa. Kama kikifika
kiangazi, huwa unapungua maji, yanakuwa machache. Kama maji yakipungua
watu wanaanza kulima humo mwenye bonde la mto huo. Wanalima maharagwe,
mchicha, mahindi ya kiangazi na vitu vingi. Kila mtu mbegu anayopenda
kulima.
Kwa hiyo kazi za mto huu ni nyingi. Huwezi kuzisema
zote ukamaliza, hapana. Ila utakazoweza kusema ndiyo utasema kama hizi
nilizosema. |
|
|
|
Maghambo mahya /Msamiati
|
mukeema, bhakeema |
mwanamke, wanawake |
-bhumbika monga |
-jaa mto |
-gholelela mansi |
-mwagilia maji |
iikata, makata |
bonde, mabonde |
iisembe, masembe |
samaki |
iisyubha, masyubha |
jua, mchana |
-kansa |
-fua |
kusogho |
masika |
kutunde |
juu ya mto au njia |
kwifo |
chini |
-lima |
-lima |
-lobha / -nyahula masembe |
-vua samaki |
mansi ghaa kunywa |
maji ya kunywa |
mbuto |
mbegu |
monga, myonga |
mto, mito |
mugholo |
jioni |
nsonfi |
kambare |
-nyaagha |
-oga |
-seeha |
-pungua |
sihwa |
kiangazi |
-sunga |
-ogelea |
-taha (mansi) |
-chota/-teka maji |
-tunga |
-chunga |
|
|
|
Copyright 2016 (c) Yuko ABE, All rights reserved. |