This site offers materials from Bende, Katavi Region, Tanzania
 IRC & LingDy 2
ILCAA, Tokyo University of Foreign Studies

Home Introduction Tusahule Sibhende
Dictionary

Unit 5  Suula jya bhutaanu

Malwele / Magonjwa

Malwele ghaa bhatwana / Magonjwa ya Watoto

Ghooghu mwana ghaakafuukanga no bhulwele. Alina Nsuko ne Ngili. Ahensile kufelwa kwa mufumo akakolelwe. Kubha no kuhensa kumanya, mukunge mumutumba. Kubha naalino bhoosa, kabhili ne myansi mumutwe kutananala. Halafu ne mpuka mundaa kujughuma, manya ni jyejo ndwala. Fela bhwangu kwa mufumo.


Huyu mtoto alizaliwa na ugonjwa. Ana “nsuko” na “ngili.” Anatakiwa kupelekwa kwa mganga wa kienyeji akatibiwe. Kama unataka kujua mwangalie mwilini. Kama ana manyoya na mishipa ya kichwani imesimama. Halafu na chango tumboni linaunguruma, ujue ni huo ugonjwa. Peleka haraka kwa mganga.


Malwele ghaa sighoosi "Musipa" / Magonjwa ya wanaume "Mshipa"
Musipa ni bhulwele bhukoolwala bhaghoosi. Musipa ghulina nsila singi. Hali mpuka, ao kuhala. Handi hali Musipa ghwa kukwesa ao kusoosya. Ghooghu ghwa kusoosya kubha ghwabha no mukosi, ghwalwala iihagha. Ghwa kutansya ghwene teghukootinsya kwihagha. Handi ghukoojighala masu ao kunia. Handi fyonse hamwi. Kubha ghwatinda kukolelwa ghwafwa.

“Mshipa” ni ugonjwa wanaougua wanaume. Mshipa una njia nyingi. Pana chango au kuharisha. Pengine pana mshipa wa kuvuta au kuteremka. Huu wa kushuka kama ukiwa na mkosi, unaugua busha. Wa kupandisha wenyewe haukawizi kuua. Pengine unafunga mkojo au kunya. Pengine vyote pamoja. Kama ukikawia kutibiwa unakufa.


Malwele ghaa sikeema "Lyamunda" / Magonjwa ya wanawake "Lyamunda"

Ndwala jya Lyamunda jikoolwala bhakeema. Jyene ni mundaa kukokota. Yaani mwabha kobhe muli sintu sili kupala. Na agho jihensilwe kukolelwa bhwangu. Handi bhakookolela bhanasilika. Hakukabha nasikalwali kabhili.

Ugonjwa wa “Lyamunda” huwa wanaugua wanawake. Wenyewe ni tumbo kukokota. Yaani (tumboni) mnakuwa kama mna kitu kinaparua. Nao unatakiwa kutibiwa haraka. Pengine wanatibia kwa kuzindika. Ili asiugue tena.
Masiina ghaa malwele /Majina ya magonjwa

bhuhele upele
bhulwele, malwele ugonjwa
bhusasi kichaa
-fuma kafita -tokwa jasho
-fuma malaso -tokwa na damu
-fimba -vimba
-hala -harisha
iihagha busha
iihima ugonjwa wa watoto, dalili yake ni homa
kahweka ambizi ya minyoo
kalembe, katuuta surua
-lwala -wa mgonjwa, -umwa
mahunsi mafua
maleelia malaria
munoghe damu inayotoka puani
mpungu degedege
mulwele, bhalwele mgonjwa, wagonjwa
ndolobho malale
ngili mtoto njiti 
nsuko mtoto aliyezaliwa bila nywele mwilini, mtoto njiti
-sala wehuka 
silonda, filonda wehuka kidonda
sisekwas kilema, mwenye ulemavu
 

Fitambo /Mwili 

 

bhujenje vinyweleo, nywele za mwili kughulu, maghulu mguu, miguu
iijungo, majungo goti, magoti liinso, meenso jisho, macho
iikosi shingo lukasa kiganja
iikumo, makumo kidole, vidole luko kisogo
iikumo nsilo kidole gumba lupambala unyayo
iitako, matako tako, matako mankwaha makwapa
iitamba, matamba paja mughongo mugongo
iitundu kifua mulomo mdomo
iitwi, matwi sikio, masikio munyonyo kitovu
kakookola kiwiko mutwe, mitwe kicha, vichwa
kasafu migu wachini kuanzia goti ndaa tumbo
kasinsila kisigino nyele nywele
kakosogolo kifundo nyiindo pua
kughoko, mabhoko mkono, mikono
 

Copyright 2016 (c) Yuko ABE, All rights reserved.