This site offers materials from Bende, Katavi Region, Tanzania
 IRC & LingDy 2
ILCAA, Tokyo University of Foreign Studies

Home Introduction Tusahule Sibhende
Dictionary

Unit 16  Suula jye ekumi na mukaagha

Kamughyenyi

Kamughenyi kee ebhubha lya mukeema / Hadithi ya mwanamke mwenye wivu

Ghundi na agho, akabheele natungile musya. Ghoogho musya ghaaswaana tu ne ebha. Kundi bhoghaaswana ne ebha, mukasi isiimi no ghoogho musya. Isiimi mukufyala bhaafyalila twa hamwi. Kundiinu ghooghu mukasi abhwene mwegho ghwalwasya, ghaabhaleetye,
-- Twala mwana.
Na agho,
-- Ti ndakumutwala bhuti, no one ndina mwana.
Kundi ghaatwala mwana. Ghaafika mumonga ghaasumpukisya ghwake ghooghu musya ghwabho. Na agho lili tu mwikosi.
Lufuku lobhaakaleetanga bhwenge, obhwalaakubha na agho,
-- Ti kateeke makoma.
Na agho ghaatwala tu ghooghu mwana ghwakeesye ebhusya, ghaaja kuputaghula mwana heefo makoma kulughamba. Kundi haaho ghaaja no kungoma ghaatwala ne elegho kumughongo ghaaheeka.
Kundi bhoghaaheeka bhwalaakufike elo mungoma ghooghu musya,
-- Fikoojela no monga ne fikoosigha na makoma fisogha fihee, bhaama-bhusya?
-- Fisogha fyonse muntu ghwane, tyajinsi ti bhaajihagha mwanaaje.
Kundi kabhili,
-- Fikoojela no monga ne fikoosigha na makoma fisogha fihee, bhaama-bhusya?
-- Fisogha fyonse muntu ghwane, tyajinsi ti bhaajihagha mwanaaje.
-- Kabhasabhulile bhatwana makoma ghaagha gha sinya akale?
Ghaafika ghaaja tu kusabhula. Kundiie ghanatoloka ghoogho musya, obhwalaakwiseelo,
-- Nyansala ukali hee?
Ghaajilukanga no ghooghu, ghuleegho ghaaheekula ghwabheele naaheekile, ghaaghuleka. Kuja tyakasabhule tu umutwe ghwake mwanaaje, ghaajitaghilako.
-- Uune kubha mwaja mwamulola Nyansala, musimuleeti hanu. Mwamwihaghila kookoe.
Kundi mulaabho iibha ghaabhuuka abhaliite kuja kamwihagha, kundi ghaasangaana tu no mukeekulu,
-- Ujiile hee?
Na agho,
-- Ti njiile mukeehagha Nyansala ghaakaputaghula mwana.
Na agho,
-- Ti ghwamuleeta kubhwami koghwamuleeta.
Kundi ghaamusangana ne ekulya tu majoobha tu ghaakusya ‘mba’ ghaakusya.
-- Njihaghile hanue.
Kakabheele kanya Lwambuko.
-- Njihaghile hanu, taata-bhusya.
Na agho,
-- Ti tuje kulugho, kaafika kulugho, ghookuja haaho habhwami.
-- Mwakeela sii?
-- Uune nankeehagha mwanaaje. Uunyene ghaakasumpukisyanga mwanaane, no one mwanaaje namputaghula nanteeka.
-- Ti leka uune nsyakasumpukisyanga. Bhukabhe elyo kaleenu.
Bhaaja bhaakakaleeta,
-- Gho onyene ghoogho.
Kundi musya ghaasiibha natoosilweho.


Bwana moja tajiri alikuwa amefuga mtumwa (aliyeitwa Nyansala). Huyo mtumwa akatongozwa na tajiri wake. Alivyotongozwa na huyu bwana, ikatokea mke wake akapata mimba na huyo mtumwa akapata mimba. Mke na mtumwa walizaa katika kipindi kimoja. Mke wa roho ikamuuma, mke akamwambia mtumwa,
-- Chukua mtoto.
Naye akamjibu,
-- Nitamchukuaje na mimi nina mtoto?
Kisha mwanamke tajiri akachukua mtoto wa mtumwa. Akafika mtoni akamtumbukiza mtoto wa yule mtumwa wao. Naye mtoto wake alimbeba shingoni.
Siku moja kulikuwa harusi ya fulani, ndipo na yeye mwanamke akamwambia mtumwa,
-- Nenda kapike magimbi.
Mtumwa akachukua yule mtoto wa mwanamke akaanza kumkatakata, mtoto chini magimbi juu. Halafu akaenda ngomani huku amebeba kibuyu mgongoni.
Mtumwa alifika ngomani na kibuyu chake mgongoni, akamuuliza tajiri wake,
-- Vinavyokwenda na mto na vinavyoungua na magimbi vizuri vipi, tajiri wangu?
(Yule mwanamke bila kujua kuwa yule mtumwa ameua mtoto wake akajibu)
-- Vizuri vyote mtu wangu.
Mtumwa akauliza tena,
-- Vinavyokwenda na mto na vinavyoungua na magimbi vizuri vipi tajiri wangu?
-- Vizuri vyote mtu wangu.
Mtumwa akasema,
-- Kawatolee watoto magimbi yale ya kizamani?
Mwanamke akafika akaanza kuopoa. Halafu mtumwa akatoroka, ndiyo akaja sasa yule mwanamke,
-- Nyansala uko wapi?
Nyansala alikuwa ameshakimbia, lile likibuyu alilokuwa amebeba aliliacha pale. Mwanamke akaenda kuopoa akaona kichwa cha mtoto wake, akaangua kilio, akasema,
-- Mkimwona Nyansala msimlete hapa. Mmuue huko huko.
Asubuhi mume wake akaondoka kwenda kumuua Nyansala, njiani akakutana na mzee, akamuuliza,
-- Unaenda wapi?
-- Naenda kumuua Nyansala amekatakata mtoto wangu.
-- Mpeleke kwa mtemi, ndiko umlete.
Akamkuta Nyansala anakula karanga anapasua mba, anasaga.
Nyansala, alikuwa mtu wa Ng’ambo (Congo) akasema,
-- Niue hapahapa. Niue hapa Bwana wangu.
-- Twende nyumbani.
Walipofika nyumbani halafu wote watatu wakaenda kwa mtemi. Mtemi aliwauliza,
-- Mmefanya nini?
Nyansala alijibu,
-- Mimi nimeua mtoto wake. Yeye alimtumbukiza mtoto wangu na mimi mtoto wake nikamkatakata na kumpika.
Mwanamke tajiri alijibu,
-- Hapana. Mimi sikumtumbukiza. Yupo pale.
Wakaenda wakakaleta.
-- Ndiyo yeye huyo.
Halafu mtumwa akabaki ameolewa hapohapo.



Kaakateebhekwanga ne Bi Mwamini Kajabala (kwene)
Hadithi imesimuliwa na Bi. Mwamini Kajabala (kulia)

Copyright 2016 (c) Yuko ABE, All rights reserved.